New York. Iran yapewa muda hadi mwishoni mwa August.
29 Julai 2006Wanachama watano wakudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa pamoja na Ujerumani wamefikia makubaliano juu ya muswada wa azimio ambalo litaipatia Iran hadi mwishoni mwa mwezi wa August kuweza kusitisha zoezi lake la kurutubisha madini ya uranium ama itakabiliwa na kitisho cha vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia.
Muswada huo umeanza rasmi kusambazwa kwa wajumbe 15 wa baraza hilo. Balozi wa Marekani John Bolton amesema kuwa kura inaweza kupigwa mapema wiki ijayo.
Balozi wa Russia Vitally Churckin , amesisitiza kuwa azimio hilo jipya halitatishia kuiwekea vikwazo Iran na kwamba ni wito kwa Iran kuingia katika majadiliano.
Iwapo Iran haitajibu, baraza la usalama litafikiria kuweka vikwazo.