New York. Baridi kali itazuwia utoa misaada Pakistan.
29 Oktoba 2005Wataalamu wa hali ya hewa wa umoja wa mataifa wanasema kuwa hali ya hewa ya baridi kali na barafu pamoja na theluji ambayo kwa kawaida inaanguka kwa wingi , hivi karibuni itaanza katika maeneo ya jimbo la Kashmir nchini Pakistan na kuhatarisha juhudi za kuwapatia chakula na makaazi watu walionusurika katika tetemeko la ardhi ambalo limelikumba eneo hilo mapema mwezi huu.
Mashirika ya kutoa misaada pia yametoa tena wito wa kupatiwa fedha zaidi ili kuweza kuendelea na juhudi za kutoa misaada kwa mamilioni ya watu ambao wameachwa bila makaazi na tetemeko hilo la ardhi lililotokea hapo Oktoba 8.
Licha ya kufanyika kwa mkutano mkubwa wa wafadhili mjini Geneva mapema wiki hii, umoja wa mataifa unasema kuwa upungufu mkubwa wa fedha unatishia kuingilia kati juhudi hizo za kutoa misaada.
Ujerumani imetoa ahadi ya kutoa Euro milioni 5.5 zaidi katika juhudi hizo za uokozi. Kiasi hicho ni nyongeza katika Euro milioni 20 ambazo Ujerumani imekwisha toa.