New York. Baraza la usalama kupiga kura leo kuhusu Iran.
23 Desemba 2006Matangazo
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepanga kupiga kura leo kuhusu vikwazo dhidi ya Iran kuhusiana na nia yake ya kujipatia teknolojia ya kinuklia.
Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zimesambaza muswada ambao umefanyiwa mabadiliko ambao unalenga kupata uungwaji mkono wa Russia kwa ajili ya viwazo hivyo.
Msemaji wa Russia ameueleza muswada huo kama hatua kuelekea mbele.
Azimio hilo litazitaka nchi zote kupiga marufuku kuipatia Iran mada maalum pamoja na teknolojia ambao itafanikisha mpango wa Iran wa kinuklia pamoja na uwezekano wa kutengeneza mabomu.
Tehran imesema kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani.