MigogoroMashariki ya Kati
Israel: Tuna matumaini ya kufikiwa mpango wa kuachiwa mateka
11 Julai 2025Matangazo
Netanyahu ameeleza kuwa mateka 50 ndio bado wako mikononi mwa kundi hilo, na 20 ndio bado wapo hai, huku akiongeza kuwa kuna uwezekano Israel na Hamas wakaafikiana pia juu ya mpango wa usitishaji mapigano kwa siku 60, makubaliano ambayo amesema yanaweza kutumiwa na pande hizo mbili ili kujaribu kuvimaliza kabisa vita vya Gaza.
Wakati Alhamisi usiku watu 66 wakiripotiwa kuuawa huko Gaza, kundi la Hamas limesema bado kuna masuala kadhaa ambayo hayajapatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na mtiririko wa misaada, kuondolewa kwa vikosi vya Israel huko Gaza na kuumaliza kabisa mzozo huo.