Netanyahu na Trump wajadili kuhusu mateka wa Gaza na Hamas
9 Julai 2025Matangazo
Katika taarifa, Netanyahu amesema kuwa wakati wa mazungumzo yake na trump, alilisisitiza kuhusu malengo ya Israel.
Trump akutana kwa mara pili na Netanyahu Ikulu Marekani
Netanyahu pia amesema wamekuwa na kikao kifupi na Makamu wa Rais JD Vance ambapo wamezingatia juhudi za kuwakomboa mateka wa Israel na kwamba hilo linawezekana kwa sababu ya shinikizo la kijeshi linalowekwa na askari wao mashujaa.
Trump: Kundi la Hamas linataka kusitisha vita Ukanda wa Gaza
Mkutano huo wa Jumanne ulikuwa wa pili katika muda wa saa 24 kati ya viongozi hao wawili, huku Trump akizidisha shinikizo kwa Netanyahu kufikia makubaliano ambayo yanaweza kumaliza kile alichokiita "janga" la vita huko Gaza.