Netanyahu: Israel haiyakubali mapendekezo ya Hamas
6 Julai 2025Matangazo
Netanyahu amenukuliwa na Shirika la Habari la DPA, akisema mabadiliko ambayo Hamas inataka kuyafanya katika pendekezo la Qatar yaliofikishwa kwao usiku wa jana hayakubaliki kwa Israeli. Maafisa wa Hamas waliiambia DPA kuwa bado kuna haja ufafanuzi kuhusu kuendelea kwa usitishaji mapigano baada ya kipindi cha awali cha siku 60, kuondolewa kwa wanajeshi wa Israel Gaza na upatikanaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo pasina vikwazo. Mazungumzo hayo yanayoratibiwa na Qatar, Misri na Marekani yanalenga kufanikisha makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku 60 huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas, na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel.