Netanyahu kukutana na Trump mjini Washington wiki ijayo
1 Julai 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atakutana na rais wa Marekani, Donald Trump, mjini Washington Julai 7.
Taarifa hiyo imeripotiwa jana Jumatatu na vyombo kadhaa vya habari vya Israel. Awali hakukuwa na taarifa rasmi ya serikali ya Isreal kuthibitisha kufanyika kw amkutano huo.
Msemaji wa rais Trump Karoline Leavit alikuwa amesema katika mkutano wa waandishi habari mapema Jumatatu kwamba Netanyahu alikuwa ameonesha nia ya kukutana na rais Trump mjini Washington, na walikuwa wanapanga tarehe ya mkutano.
Tayari Trump alimkaribisha Netanyahu katika ikulu yake mjini Washington mwezi Aprili na kama kiongozi wa kwanza wa kigeni katika awamu yake mpya kama rais mnamo Februari.