Netanyahu kujadili na Trump "ushindi dhidi ya Hamas"
3 Februari 2025Kabla ya kuanza ziara hiyo, Netanyahu aliwaambia waandishi wa habari kwamba atakapokutana na Trump hapo kesho, atajadili kuhusu ushindi dhidi ya Hamas, kupambana na Iran na kuwaachilia mateka wote.
Trump amwalika Netanyahu Ikulu ya White House
Netanyahu ameongeza kuwa hii itakuwa mara ya kwanza kwa Trump kukutana na kiongozi wa kigeni tangu arejee Ikulu ya White House mwezi Januari, kipaumbele ambacho Netanyahuamesema kinaashiria mengi na kwamba anadhani ni ushuhuda mkubwa wa muungano wa Israel na Marekani.
Mkutano utaimarisha muungano wa kina kati ya Israel na Marekani.
Alipowasili nchini Marekani jana usiku, Netanyahu alilakiwa na balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Danny Danon, ambaye alisisitiza kuwa mkutano ujao kati ya Trump na Netanyahu utaimarisha muungano wa kina kati ya Israel na Marekani.
Netanyahu akabiliwa na shinikizo la kuidhinisha makubaliano
Trump, ambaye amejisifu kwa kuwezesha kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya miezi 15 ya vita, amesema jana kwamba mazungumzo na Israeli na nchi zingine za Mashariki ya Kati yanaendelea.
Ofisi ya Netanyahu imesema kwamba ataanza mazungumzo na mjumbe maalumu wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati Steve Witkoff hii leo kuhusu masharti ya awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Jeshi la Israel laripua takriban majengo 20 katika kambi ya Jenin
Shirika rasmi la habari la Palestina WAFA, limeripoti jana kuwa wanajeshi wa Israel waliripua kwa wakati mmoja takriban majengo 20 katika sehemu ya mashariki ya kambi ya wakimbizi ya Jenin, na kuongeza kuwa milipuko hiyo ilisikika katika jiji lote la Jenin na sehemu za miji jirani.
Baraza la Israel kupiga kura kuhusu kusitisha mapigano Gaza
Mkurugenzi wa hospitali ya serikali ya Jenin Wisam Baker, ameliambia shirika hilo la WAFA kwamba sehemu ya hospitali hiyo imeharibiwa lakini hakukuwa na majeruhi.
Wizara ya afya ya Palestina imesema kuwa jeshi laIsraellimemuua mzee mmoja wa miaka 73 na mwanamume wa umri wa miaka 27 katika matukio tofauti katika Ukingo wa Magharibi hapo jana.
Iran yalaani pendekezo la kuwahamisha Wapalestina
Iran leo imelaani pendekezo la Trump la kuwahamisha Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza, na kuonya kuwa itakuwa sawa na safisha safisha ya kikabila.
Ofisi ya Netanyahu yakanusha Hamas kukubali pendekezo la kusitisha vita
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmaeil Baqaei, amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuwasaidia Wapalestina kupata haki yao ya kujitawala badala ya kushinikiza mawazo mengine ambayo yatakuwa sawa na safisha safisha hiyo ya kikabila.