Netanyahu kujadili na Trump "ushindi dhidi ya Hamas"
3 Februari 2025Matangazo
Mkutano huo wa kesho kwenye Ikulu mjini Washington utakuwa ni wa kwanza kwa rais Trump na kiongozi wa kigeni tangu mwanasiasa huyo aliporejea madarakani kuiongoza Marekani kwa muhula mwingine mwezi uliopita.
Utafanyika katika wakati wapatanishi wa Marekani na mataifa ya kiarabu wanafanya matayarisho ya duru mpya ya mazungumzo kwa dhima ya kurefusha makubaliano ya kusitisha vita kwenye Ukanda wa Gaza.
Soma pia:Jeshi la Israel lalipua majengo kadhaa Jenin
Hivi sasa Israel na kundi la Hamas wanatekeleza mkataba wa kusitisha mapigano kwa wiki sita ambao umewezesha kuachiwa huru kwa mateka 18 wa Israel na mamia ya Wapalestina waliokuwa wamefungwa jela.