Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kukutana na Trump
7 Aprili 2025Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anajiandaa kuanza ziara yake Ikulu ya White House leo Jumatatu, kwa mara ya pili tangu rais Donald Trump alipoingia madarakani mwezi Januari.Netanyahu kujadili na Trump "ushindi dhidi ya Hamas"
Netanyahu ambaye atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Trump, baada ya tangazo lake viwango vipya vya ushuru duniani , amesema watajadili kuhusu juhudi za kuwarudisha nyumbani Israel, mateka wanaoendelea kushikiliwa katika Ukanda wa Gaza.Vita kati ya Israel na Hamas vimeingia mwezi wa saba
Lakini pia watazungumzia kuhusu Iran,warranti uliotolewa na mahakama ya kimataifa ya jinai ya ICC dhidi ya Netanyahu pamoja na suala la ushuru. Israel ambayo ni mshirika muhimu wa Marekani pia haikuepuka kuwekewa ushuru vilivyotangazwa wiki iliyopita na Trump.