SiasaMarekani
Netanyahu kuzuru White House wiki ijayo
1 Julai 2025Matangazo
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika huku kiongozi huyo wa Marekani akizidisha mbinyo kwa serikali ya Israel na Hamas ili kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuvimaliza vita huko Gaza.
Ziara hiyo imethibitishwa na serikali zote mbili kupitia maafisa ambao walizungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwa kuwa hawakuwa na idhini ya kuzungumzia hilo hadharani.
Hii itakuwa ni ziara ya tatu ya Netanyahu mjini Washington tangu Trump alirudi madarakani mwezi Januari, na inafanyika baada ya Marekani kujiingiza kwenye vita kati ya Israel na Iran kwa kushambulia maeneo ya nyuklia ya Iran.