Netanyahu ataka Israel iiangamize Hamas ili kuachiwa mateka
5 Agosti 2025Kauli hiyo ameitoa Jumanne wakati alipozuru chuo cha mafunzo ya kijeshi, kabla ya mkutano unaotarajiwa wa wakuu wa usalama kuzungumzia mipango ya vita vya Gaza.
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa Netanyahu anatarajiwa kukutana na mkuu wa majeshi na waziri wa ulinzi Jumanne jioni, na inadaiwa huenda kiongozi huyo akaamuru kukaliwa kimabavu ardhi yote ya Palestina.
Wakati huo huo, Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kiutu, OCHA, Jens Laerke, amesema Gaza inahitaji mamia ya malori zaidi ya misaada.
''Misaada imeingia, unajua, malori kadhaa yanaingia kwa siku, si ndiyo? Mahitaji ndani ya Gaza ni kwamba inapaswa kuwa na mamia kwa mamia zaidi ya malori, sio tu kila siku, kila wiki, lakini kwa miezi na labda kwa miaka ijayo,'' alisisitiza Laerke.
Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, Larke amesema mahitaji ya Gaza ni makubwa na kwamba kuna watu wanaokufa kwa njaa kila siku.