Netanyahu ashtumiwa kwa matamshi kuhusu mauaji ya Armenia
27 Agosti 2025Matangazo
Wizara hiyo ya mambo ya nje ya Uturuki, imesema taarifa ya Netanyahu kuhusu matukio ya mwaka 1915 ni jaribio la kutumia mikasa ya zamani kwa sababu za kisiasa.
Wizara hiyo imejibu madai ya Netanyahuyaliyosema kwamba mauaji ya Waarmenia wengi wakati wa enzi ya Vita vya Kwanza vya Dunia katika Ufalme wa Ottoman yalikuwa mauaji ya halaiki, neno ambalo Uturuki inalikataa vikali.
Armenia na Azerbaijan zalumbana upya
Taarifa ya wizara hiyo imeendelea kusema kuwa Netanyahu, ambaye ameshtakiwa kwa jukumu lake katika mauaji ya halaiki yaliyofanywa dhidi ya watu wa Palestina kwenye Ukanda wa Gaza, anajaribu kuficha uhalifu ambao yeye na serikali yake wametenda.
Israel imepuuzilia mbali tuhuma za mauaji ya halaiki huko Gaza na kuzitaja kuwa uongo mtupu.