Netanyahu asema kiongozi wa Hamas Mohammed Sinwar ameuawa
28 Mei 2025Akizungumza bungeni, Waziri mkuu huyo alijumuisha jina la Sinwar kwenye orodha ya viongozi wa Hamas waliouawa na Israel katika ukanda huo ulioharibiwa kwa vita. Mohammed ni kaka yake Yahya Sinwar, kiongozi wa Hamas na mmoja wa waliopanga shambulio la Oktoba 7, 2023, ambaye aliuawa na vikosi vya Israeli mwaka jana. Wataalamu wanasema kuna uwezekano Mohammed Sinwar alichukua wadhifa wa mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas, la Ezzedine al-Qassam Brigades, baada ya kiongozi wake Mohammed Deif kuuawa.
Wakati huo huo, Shirika lenye utata la Gaza Humanitarian Foundation limetangaza kusitisha kwa muda utoaji wa msaada katika Ukanda wa Gaza kufuatia vurugu zilizozuka wakati wa ufunguzi wa operesheni zake mjini Rafah. Umati wa watu walikitivamia kituo hicho kipya kwa kuvunja kuta na kukasikika milio ya risasi. Maafisa wamesema Mpalestina mmoja aliuawa kwa riasasi na wengine 48 kujeruhiwa.