Netanyahu aapa Israel kuendelea na vita Gaza
20 Aprili 2025Na haitavimaliza vita hivyo kabla ya kuliangamiza kabisa kundi la Hamas, kuwakomboa mateka na kuhakikisha kuwa eneo hilo haliwi tena kitisho cha usalama kwa Israeli. Lakini pia Netanyahu ameirejea tena kauli yake ya kusema Iran haitafikia hatua ya kuwa na silaha silaha za nyuklia. Kwa upande wake Hamas imesema inaweza kuwaachilia mateka kwa makubaliano ya kuondoa majeshi katika ardhi yao na hatua ya kudumu kusitisha mapigano kama ilivyoainishwa katika makubaliano yaliyohitimishwa na Israel. Netanyahu yuko katika shinikizo linaloongezeka la ndani, sio tu kutoka kwa familia za mateka na wafuasi wao lakini pia kutoka kwa askari wa akiba na waliostaafu wa Israel wanaohoji hatma ya kuendelea kwa vita baada ya Israel kusambaratisha juhudi za usitishaji mapigano mwezi uliopita.