Netanyahu amteuwa mkuu mpya wa shirika la ujasusi wa ndani
31 Machi 2025Netanyahu amemteuwa Sharvit kuongoza taasisi hiyo ambayo hufuatilia na kuzuia mashambulizi kutoka kwa makundi ya wapiganaji ya Kipalestina.
Kufutwa kazi kwa Bar kulizua maandamano makubwa
Mapema mwezi huu, Netanyahu alimfuta kazi Bar, katika hatua iliyozua maandamano makubwa nchini Israeli.Netanyahualisema alipoteza imani yake kwa Bar kutokana na shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023 pamoja na kutoelewana kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano.
Mkuu wa Intelijensia Israel aachishwa kazi huku jeshi likitanua operesheni GazaLakini wakosoaji wamesema kuwa kufukuzwa kwa Bar kulihujumu taasisi huru za serikali ya Israel na kulifanyika wakati wa shida, ambapo Bar na taasisi hiyo, walikuwa wakichunguza ushirikiano kati ya Qatar na washauri wa karibu wa Netanyahu.