Netanyahu akabiliwa na shinikizo la kumaliza vita huko Gaza
24 Agosti 2025Miezi kadhaa ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Israel na Hamas hadi sasa hayajazaa matunda.Wanachama wa siasa kali za mrengo wa kulia wanaounda serikali ya mseto ya Netanyahu wanapinga vikali makubaliano yoyote na Hamas.
Waziri wa Fedha Bezalel Smotrich ametishia mara kadhaa kujiondoa kwenye muungano ulio madarakani ikiwa mpango huo utasainiwa, jambo ambalo linaweza kupelekea kuvunjika kwa serikali ya Netanyahu.
Jumamosi, Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel Benny Gantz alimtolea wito Netanyahu wa kuunda serikali ya umoja na wanachama wa upinzani katika jitihada za kuwezesha mpango wa kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa huko Gaza . Hayo yanajiri wakati mapigano yameendelea kuripotiwa huku wiki hii Umoja wa Mataifa ukitangaza rasmi kuwepo kwa baa la njaa huko Gaza.