Netanyahu aapa kuwarudisha nyumbani mateka wote
27 Mei 2025Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameapa kuwarudisha nyumbani mateka wake wote wanaoshikiliwa na Hamas, walioko hai na waliokufa.
Kauli hiyo ya Netanyahuimetolewa chini ya kiwingu cha kuweko mkanganyiko kuhusu hatma ya pendekezo la usitishaji mapigano kwa siku 70, hatua ambayo ilitarajiwa kutowa nafasi ya kuachiliwa mateka 10 wa Israel pamoja na wafungwa wa Kipalestina.
Jana kundi la Hamaslilisema limeridhia pendekezo jipya la usitishaji vita lililotolewa na mjumbe wa Marekani Steve Witkoff, lililowasilishwa na wajumbe, hata hivyo baadae msemaji wa Witkoff alikanusha kwamba Hamas wamekubali pendekezo hilo.
Watu takriban 52 wameuwawa katika Ukanda waGazakwa mujibu wa timu ya waokoaji kwenye Ukanda huo ambako jeshi la Israel limeendelea kushambulia. Jeshi la Israel limesema leo, limezuia makombora yaliyofyetuliwa kutoka Yemen na waasi wa Kihouthi.