MigogoroIsrael
Netanyahu aahidi kuwaondoa wanajeshi wake Lebanon
25 Agosti 2025Matangazo
Taarifa ya ofisi ya Netanyahu imesema ikiwa Jeshi la Lebanon (LAF) litachukua hatua zinazohitajika
kuwapokonya silaha Hezbollah, Israel itashiriki hatua za kubadilishana, na kuwapunguza kwa hatua wanajeshi wake, chini ya uratibu wa Marekani.
Israel bado ina wanajeshi kwenye vituo vitano kusini mwa Lebanon, wanaoendelea kufanya mashambulizi na kuwaua raia nchini humo karibu kila siku, likisema linawalenga Hezbollah.
Hezbollah inayoungwa mkono na Iran imesema itakubali kupokonya silaha wanamgambo ikiwa Israel itasitisha mashambulizi nchini Lebanon na kuwaondoa wanajeshi wake waliosalia kusini mwa nchi hiyo.