Katika mfululizo wa Makala za video zilizoandaliwa na DW, tunatizama jinsi gani ukoloni wa Ujerumani Afrika ulivyokabiliwa na upinzani mkali. Nduna Mkomanile ambaye alijitahidi kuziunganisha jamii za Tanzania dhidi ya ukoloni wa Wajerumani wakati wa vita vya Maji Maji mwanzoni mwa karne ya 20. Sasa anatambulika kama mmoja wa mashujaa wa kike muhimu zaidi wa uhuru wa Tanzania.