NDJAMENA : Watesaji wa Chad hawakufikishwa mbele sheria
13 Julai 2005Matangazo
Shirika la kutetea haki za binaadamu linasema kwamba watesaji wa zamani wanaendelea kushikilia nyadhifa za serikali nchini Chad.
Shirika la Human Right Watch lenye makao yake mjini Marekani limesema kwamba zaidi ya washirika 40 wa dikteta wa zamani Hissene Habre ambaye aliitawala Chad kuanzia mwka 1982 hadi mwaka 1990 bado wanashikilia nyadhifa za juu serikalini licha ya wengi wao kushutumiwa kwa kutesa na kuuwa na Tume ya kutafuta Ukweli ya nchi hiyo.
Repoti ya shirika hilo inasema kwamba maelfu ya wahanga chini ya utawala wa Habre katu hawakuwahi kupatiwa fidia au kutambuliwa na serikali ya sasa ya Chad.