NDJAMENA: Mapatano ya amani nchini Chad
20 Agosti 2005Matangazo
Serikali ya Chad kwa mara ya tatu imetia saini mapatano ya amani pamoja na waasi wa kaskazini katika kipindi cha miaka mitatu.Kuambatana na mkataba huo wa amani kati ya chama cha MDJ na serikali,imekubaliwa kuwaachilia huru wafungwa wa vita,kuwajumuisha waasi wa zamani serikalini na katika vikosi vya usalama na pia eneo lenye mabomu yaliozikwa ardhini,lisafishwe.