NDJAMENA Chad kubadili katiba
22 Juni 2005Matangazo
Wapigaji kura wa Chad wameunga mkono kuibadili katiba ya taifa lao kupitia kura ya maoni, hivyo kumruhusu rais wa sasa kugombea wadhifa wake kwa kipindi kingine cha tatu. Zaidi ya asilimia 77 ya wapigaji kura hao walipiga kura ya ndio kumruhusu rais Idriss Deby kushiriki katika kinyang´nyiro cha uchaguzi mwaka ujao wa 2006.
Kamanda huyo wa zamani wa jeshi alinyakua madaraka katika taifa hilo la Afrika ya Kati miaka 15 iliyopita kabla kushinda uchaguzi wa mwaka wa 1996 na 2001. Deby amekanusha madai kwamba anataka kuwa rais wa taifa hilo hadi atakapofariki na kwamba anamuandaa mwanawe kuwa mrithi wake.