JangaAfrika
Ndege yaanguka na kuua watu 20 nchini Sudan Kusini
29 Januari 2025Matangazo
Waziri wa Habari wa Jimbo la Unity Gatwech Bipal amesema ndege hiyo ilianguka kwenye uwanja wa ndege wa Unity asubuhi ya leo Jumatano wakati ikiondoka kuelekea mji mkuu Juba.
Bipal amesema abiria walikuwa ni wafanyakazi wa kampuni ya mafuta ya greater Pioneer Operating, GPOC, inayojumuisha Shirika la Mafuta la Kitaifa la China pamoja na Shirika la Mafuta la Nile linalomilikiwa na serikali.
Amesema, miongoni mwa waliokufa ni raia wawili wa China na mmoja wa India, ingawa hakutoa taarifa za kina kuhusiana na chanzo cha ajali hiyo.