SiasaVenezuela
Wahamiaji wa Venezuela waliotimuliwa Marekani wawasili
11 Februari 2025Matangazo
Venezuela ilituma ndege mbili kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani wahamiaji karibu 200 wasio na vibali kutoka Marekani. Ndege hizo zilitumwa baada ya Rais Nicolas Maduro anayetafuta kukomesha vikwazo vya Marekani, kukubaliana na mjumbe maalumu wa rais wa Marekani mwishoni mwa mwezi uliopita, juu ya kurejeshwa kwa wahamiaji waliofukuzwa. Venezuela inatafuta kurekebisha uhusiano wake uliodorora na Marekani. Trump ameahidi kutekeleza kampeni kubwa zaidi ya kuwatimua mamiliaoni ya wahamiaji wasio na vibali katika historia ya Marekani, wengi wao kutoka mataifa ya Amerika Kusini.