NCHI ZOTE ZAKARIBISHWA KUIJENGA IRAQ:
19 Desemba 2003Matangazo
BERLIN: Wajumbe wa Baraza Tawala la Wairaqi,wamewasili Berlin wakitangaza kuwa makampuni kutoka "nchi zote" yanakaribishwa kusaidia kulijenga taifa lao.Wajumbe hao waliowasili siku ya Alkhamis walitamka maneno hayo licha ya wizara ya ulinzi ya Marekani kupinga kutoa kazi kwa mataifa yaliovipinga vita vya Iraq,kama vile Ujerumani.Mkuu wa Baraza hilo la serikali ya mpito ya Iraq,bwana Abdul Aziz al-Hakim amesema,Iraq itaweza kunufaika kutokana na ujuzi wa viwanda vya Kijerumani vilivyowahi hapo awali kufanya kazi nchini Iraq.Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair kwa mara nyingine tena wameahidi kusamehe sehemu ya deni kubwa la Iraq kwa nchi hizo mbili.Matamshi hayo yametolewa wakati ambapo mjumbe wa Marekani James Baker amekamilisha ziara yake mjini Moscow kwa kukutana na Rais wa Russia Vladimir Putin.Russia ni mkopeshaji mkuu wa Iraq,lakini nayo pia sasa yaonyesha kuwa ipo tayari kufanya majadiliano kuhusu malipo ya madeni.