Nchi za kiarabu zalaani operesheni za Israel huko Gaza
17 Mei 2025Viongozi wa nchi za Kiarabu wakiwa kwenye mkutano wao wa kilele mjini Baghdad wametoa wito leo Jumamosi wa kusitishwa mara moja kwa vita katika Ukanda wa Gaza, wakiishutumu vikali Israel kutokana na operesheni zake huko Gaza.
Wimbi jipya la mashambulizi ya Israel limesababisha vifo vya mamia ya watu tangu kusambaratika mwezi Machi, kwa makubaliano ya usitishaji mapigano na kuachiliwa kwa mateka.
Rais wa Misri Abdel-Fatah al-Sisi, ambaye nchi yake ni moja ya wapatanishi wakuu katika mazungumzo ya amani, ameikosoa Israel na kusema inafanya vitendo vya uhalifu katika ukanda wa Gaza.
Katika hatua nyingine, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema kundi la wapiganaji wa Hamas limetangaza leo kwamba linajiandaa kurejea katika duru nyingine ya mazungumzo ya usitishaji wa mapigano itakayofanyika nchini Qatar.