SiasaUkraine
EU yakosoa hatua ya Zelensky kuhusu kupambana na ufisadi
23 Julai 2025Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul amesema hatua hiyo itafanya iwe vigumu kwa Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Wakati Benjamin Haddad, Waziri wa Masuala ya Ulaya wa Ufaransa akisema kuwa Zelensky hajachelewa kutengua uamuzi huo. Rais huyo wa Ukraine ameahidi kuwasilisha mpango mpya wa kupambana na ufisadi . Hatua hiyo ya Zelensky ilizusha maandamano makubwa mjini Kiev.
Wakosoaji wanasema sheria hiyo inamlimbikizia madaraka Zelensky na itairuhusu serikali kuingilia kati kesi za rushwa zinazowahusu viongozi wa vyeo vya juu na wenye haiba kubwa katika jamii.