Nchi masikini zakabiliwa na madeni makubwa ya China
27 Mei 2025Matangazo
Shirika moja la utafiti la Australia limetowa ripoti, inayosema mataifa masikini kabisa duniani yanakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni huku kiwango cha urudishaji madeni hayo kwa mkopeshaji wake Chinakikivunja rikodi mwaka huu 2025.
Ripoti hiyo ya taasisi ya, The Lowy iliyochapishwa leo Jumanne inasema mataifa yanayoendelea yanapambana na wimbi kubwa la ulipaji madeni na riba kwa China na yataendelea kuwa katika hali hiyo kwa muongo mzima.
Wizara ya mambo ya nje yaChina imesema haina uelewa wa kina juu ya ripoti iliyotolewa, lakini imefafanuwa kwamba uwekezaji na ushirikiano wake kifedha na mataifa yanayoendelea ni mipango inayofanyika kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa.