Nchi kadhaa zataka kuongezwa kikosi cha kimataifa Haiti
28 Agosti 2025Matangazo
Kulingana na barua iliyoonekana na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP, nchi hizo zitaunda ''kundi la washirika'' kwa ajili ya kusimamia ujumbe huo ambao uliidhinishwa kwa mara ya kwanza na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2023 kuwasaidia askari wa Haiti kudhibiti ghasia zinazoendelea katika nchi hiyo.
Barua hiyo imeeleza kuwa kikosi cha MSS, hakina rasilimali za kutosha na uwezo wa kupambana na changamoto inayoongezeka.
Barua hiyo imesainiwa na Marekani, Canada, El Salvador, Guatemala, Jamaica, Kenya na Bahamas.
Nchi hizo zimesema kikosi kilichoongezwa na kuidhinishwa kufanya operesheni za kukabiliana na magenge ya uhalifu, ndicho kitaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa magenge hayo kudhibiti maeneo mengi ya Haiti.