Nchi jirani zakhofia mgawanyiko wa Iraq
15 Februari 2004Matangazo
KUWEIT CITY: Katika mashauriano yao kuhusu usalama wa kimkoa nchi jirani za Iraq zimesema zinatiwa wasi wasi na kitisho cha kuweza kugawanyiko nchi hiyo. Baada ya kumalizika vita na kuangushwa utawala wa Saddam Hussein Iraq inapaswa iwe nchi huru iliyoungana, zilisisitiza nchi hizo jirani za Iraq. Nchi hizo zisema kuwa katika mkutano wa kilele wa nchi za Kiarabu hapo mwezi ujao zitashauri zianzishwe juhudi za misaada kwa Iraq iliyoteketezwa vitani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Hoshjar Sebari alisema Iraq mpya lazima ijengeke juu ya misingi ya kidemokrasi, vyama vingi na haki za binadamu. Nchini Iraq waliuawa watu 27 na kujeruhiwa zaidi ya 35 hapo jana watu wasiojulikana walipokishambulia kituo cha polisi mjini Falluja. Jengo hilo lililokuwa na wafungwa miya kadha lilishambuliwa na makombora na mabomu ya mkono.